Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kuunda mkakati mpya kwa ajili ya maendeleo

Umoja wa Mataifa kuunda mkakati mpya kwa ajili ya maendeleo

Wakati wa kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo, litakalofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia kuanzia tarehe 13 Julai hadi tarehe 16, Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuunda mkakati mpya kwa ajili ya kufadhili maendeleo kwenye nchi 193.

Akizungumza na idhaa hii, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Idara ya Maswala ya Kiuchumi na Kijamii DESA, Wu Hong-Bo amesema shughuli hiyo ni chagamoto kubwa akiongeza kuwa matarajio ya kongamano hilo ni ya aina tatu.

Mosi ni mkakati kamilifu wa ufadhili, ambao utaangazia sehemu zote za maendeleo: kiuchumi, kijamii na kimazingira. Kwa nini ni mkakati wala si suluhu moja tu? Kwa sababu hatuwezi kupata suluhu moja itakayofaa nchi zote 193, Kwa sababu kila nchi ni tofauti na nyingine.”

Halikadhalika amesewa miradhi thabiti mipya ya maendeleo itatangazwa wakati wa kongamano hilo na kwamba mfumo imara wa ufuatiliaji utaundwa, ambao ulikosekana wakati wa kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia.

Hatimaye amesema matarajio hayo yakitimizwa, ndiyo ataridhika na matokeo ya Kongamano la Addis, ambayo yatakuwa msingi wa kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu yatakayoamuliwa mwezi Septemba, mjini New York.