Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa UM wakamilisha ziara kuhusu ukatili wa kingono Guinea

Wataalam wa UM wakamilisha ziara kuhusu ukatili wa kingono Guinea

Timu ya wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaofanya kazi chini ya Ofisi ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo, imekamilisha ziara ya siku mbili nchini Guinea.

Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya uungaji mkono juhudi zinazoendelea nchini Guinea za kuwawajibisha waliotenda uhalifu wa ukatili wa kingono katika uwanjwa wa soka mjini Conakry mnamo Septemba mwaka 2009.

Msemaji wa Katibu Mkuu, Farhan Haq, amewaambia waandishi wa habari kuwa, wakiwa Guinea, wataalam hao walikutana na Waziri wa Haki, mashirika ya umma, mawakili wa waathirika, pamoja na jopo la majaji lililowekwa kuchunguza madai hayo

Timu hiyo itaendelea kuunga mkono kazi ya jopo hilo la majaji, ili kuhakikisha kuwa wale waliotenda uhalifu huu wanawajibishwa kisheria. Kwa usaidizi wa timu ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu 400 wamesikilizwa, na kupelekea watu 15 kushitakiwa, wakiwemo maafifa wa ngazi ya juu wa kijeshi.”