Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada zaidi ya kukuza bishara inahitajika: Mero

Misaada zaidi ya kukuza bishara inahitajika: Mero

Mkutano kuhusu uwezeshaji wa kibiashara  kwa nchi zinazoendelea ulioandaliwa na shirika la biashara ulimwenguni WTO umemalizika mjini Geneva Uswisi ambapo nchi zinazoendelea zimetaka misaada zaidi ili kuinuka katika biashara.

Katika mahojiano na idhaa  hii baada ya kuhudhuria mkutano huo wa siku tatu mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva balozi Modest Mero anaeleza namna awamu ya kwanza ya misaada hiyo ilivyosaidia nchi anayowakilisha.

(SAUTI MERO)

Hata hivyo amesema misaada zaidi inahitajika ili kuinua viwango vya biashara kwa kujenga miundombinu thabiti hatua itakayowezesha nchi zinazoendelea kujitegemea na kuondokana  na utegemezi.