Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za kujisafi shuleni huko Tanzania zaleta furaha shuleni

Huduma za kujisafi shuleni huko Tanzania zaleta furaha shuleni

Jarida maalum leo linaangazia maswala ya mazingira ya shule na usafi ndani ya shule nchini Tanzania. Nchini Tanzania, asilimia 46 tu za shule za msingi zaidi ya 60,000 zilizopo nchini humo zina huduma za maji safi na vyoo salama, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, huku Shirika hilo likieleza kwamba mazingira ya shule  yasiokuwa safi, yanazuia watoto kupata elimu bora, hasa wasichana. Ungana na Priscilla Lecomte anayekusimuliwa kinachofanywa na UNICEF Tanzania.