Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtoto mwingine auawa kwa gruneti Burundi: UNICEF

Mtoto mwingine auawa kwa gruneti Burundi: UNICEF

Ghasia zinazoendelea nchini Burundu zimeendelea kugharimu maisha ya watoto ambapo katika tukio la karibuni zaidi mtoto mmoja ameuawa kwenye shambulio la gruneti kwenye jimbo la Muyinga.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema tukio hilo linafanya watoto waliouwa katika ghasia zinazohusiana na uchaguzi huko Burundi kufikia wanane.

UNICEF imesema shule mjini Bujumbura zimefungwa lakini mikoani bado zinaendelea na masomo na kwamba lazima hatua zichukuliwe kuepusha watoto kwenye ghasia.

Christophe Boulierac ni msemaji waUNICEF, Geneva, Uswisi.

(Sauti ya Boulierac)

“Kuepusha watoto kukumbwa au kushuhudia ghasia ni wajibu wa kila mtu. Tunatoa wito kwa ngazi zote za uongozi Burundi ikiweo serikali, dola na familia na serikali kutumia ushawishi wao wote kulinda watoto ili wasikumbwe na ghasia au kukamatwa na kuweka korokoroni kinyume cha sheria.”