Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSMA yalaani mashambulizi dhidi ya walinda amani Timbuktu

MINUSMA yalaani mashambulizi dhidi ya walinda amani Timbuktu

Leo, Alhamisi watu wasiojulikana wameshambulia walinda amani wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA waliokuwa doria kwenye maeneo ya Timbukutu nchini humo. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Katika taarifa yake MINUSMA imesema walinda amani 6 wameuawa, huku wengine tano wakijeruhiwa.

MINUSMA imesema kinachofanyika sasa ni operesheni za kuwapeleka majeruhi hospitalini , na askari wa zaidi wa MINUSMA wanaelekea Timbuktu kwa njia ya barabara na boti.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini humo na mkuu wa MINUSMA Mongi Hamdi amelaani vikali mashambulizi hayo akisema watekelezaji wa uhalifu huo wanapaswa kubainiwa na kupelekwa mbele ya sheria.

Ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga akiwatakia nafuu waliojeruhiwa.

Bwana Hamdi ameeleza kwamba azimio namba 2227 la Baraza la Usalama la Juni 29 mwaka huu lililoongeza muda wa mamlaka ya MINUSMA kwa mwaka mmoja limeonyesha utayari wa Baraza hilo kuwawekea vikwazo wale wanaoshambulia MINUSMA au wenye mpango wa kufanya hivyo.