Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa dharura kujadili wimbi la wakimbizi Burundi kufanyika Kenya

Mkutano wa dharura kujadili wimbi la wakimbizi Burundi kufanyika Kenya

Wakati hali ya mahitaji ya kibinadamu kwa wakimbizi wa Burundi waliosaka hifadhi nchi jirani yakizidi kila uchao, Umoja wa Mataifa na wadau wake watakuwa na mkutano wa siku moja wa kujadili udharura wa mahitaji hayo kama inavyoeleza ripoti hii ya Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Tangu kuzuka kwa sintofahamu ya kisiasa nchini Burundi mwezi Aprili mwaka huu maelfu ya raia wamemiminika nchi jirani ikiwemo Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mahitaji ya kiafya, yakizidiwa uwezo.

Sintofahamu huko Burundi imeendelea baada ya kufanyika uchaguzi wa wabunge na madiwani Jumatatu huku uchaguzi wa Rais ukipangwa tarehe 15 Julai licha ya Umoja wa Mataifa kusihi usogezwe mbele.

Sasa nchi zinazowapatia hifadhi wakimbizi zinakutana jijini Naironi kesho ambapo katika mahojiano na idhaa hii akiwa njiani kuelekea kwenye kikao hicho Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Burundi Abel Mbilinyi amesema kubwa zaidi...

(SAUTI MBILINYI)

Katika hatua nyingine Bwana Mbilinyi amesema hadi sasa hawajapokea taarifa zozote za machafuko yaliyowahusiaha wakimbzi wakati wa uchaguzi wa wabunge mapema juma hili nchini Burundi