Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa kikanda ni fursa ya kukuza kilimo Afrika Magharibi: FAO

Ushirikiano wa kikanda ni fursa ya kukuza kilimo Afrika Magharibi: FAO

Ripoti mpya kuhusu sekta ya kilimo huko Afrika Magharibi imetaja ushirikiano wa kikanda kama kichocheo kikuu kinachoweza kuimarisha sekta hiyo na hatimaye kukuza uchumi na maisha ya wananchi.

Ikitambuliwa kama Ukuaji kilimo Afrika Magharibi, vichocheo vya masoko na sera, ripoti inasema kuwa iwapo zitaimarisha ushirikiano wa kikanda, nchi hizo zitapunguza gharama na hivyo kwenda sambamba na washindani wa sekta hiyo duniani.

Frank Hollinger, mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo na pia mchumi wa FAO anatoa mfano wa ushirikiano unavyoweza kuinua kilimo..

(Sauti ya Hollinger)

“Kuoanisha itifaki za kujaribu na kupitisha mbegu mpya au aina mbali mbali za mbegu kunaweza kuharakisha upatikanaji wake katika nchi nyingine kwa kuwa sasa zitafanyiwa majaribio katika nchi moja badala ya kila nchi kufanya majaribio peke yake.”

Ripoti hiyo imeandaliwa kwa pamoja na benki ya maendeleo Afrika, FAO na jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi.