Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wakumbuka miaka 20 ya mauaji ya kimbari ya Srebenica

Umoja wa Mataifa wakumbuka miaka 20 ya mauaji ya kimbari ya Srebenica

Miaka 20 baada ya mauaji ya kimbari yaliyotokea mjini Srebrenica, nchini Bosnia na Herzegovina, kumbukizi maalum imefanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

Kwenye hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban amesema kwamba jamii ya kimataifa na umoja huo zinawajibika kwa mauaji hayo kwa kuwa zilishindwa kulinda maisha ya raia, akiongeza kuwa tangu vita vilivyosababisha mauaji hayo, mamlaka za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani zimepewa ruhusa ya kutumia nguvu ili kuzuia mauaji ya raia, na Umoja wa MAtaifa umejitahidi kuimarisha mbinu zake ili kuzuia mauaji kama hayo.

Hata hivyo amesema bado jitihada zaidi zinahitajika.

“Jamii ya kimataifa bado inashindwa kusaidia watu wengi ambao wanahitaji. Kutoka Syria hadi Sudan Kusini, watu wanakumbwa na ghasia na ugaidi. Nchi wanachama na jamii ya kimataifa wanapaswa kufanya kazi pamoja ili kujenga jamii jimuishi na kusaidia jamii zilizoathirika na ghasia kujijenga upya na kupata maridhiano.”

Mwaka 1995, zaidi ya wanaume na vijana 8,000 waumini wa dini ya kiislamu waliuawa mjini Srebrenica na vikundi vya Waserb wa Bosnia, wakati wa vita vya Balkan, kwenye mji uliobainiwa kama eneo la usalama na ambapo kulikuwa na kundi la walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Walinda amani hao hata hivyo hawakuweza kuzuia mauaji hayo kwani hawakuwa na ruhusa ya kutumia nguvu za kijeshi ili kulinda