Cuba na Marekani kufungua ofisi za ubalozi kati yao, Ban asema ni hatua murua

1 Julai 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo la leo kuwa Cuba na Marekani zitafungua tena ofisi zao za ubalozi kwenye miji mikuu ya nchi hiyo ambayo ni Havana na Washington D.C

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Ban akisema kuwa hatua hiyo ya kurejesha uhusiano wa kibalozi uliokoma zaidi ya miongo mitano iliyopita ni muhimu katika mwelekeo wa kuimarisha uhusiano kati ya pande mbili hizo.

Amesema kwa kuzingitia misingi ya katiba iliyounda Umoja wa Mataifa, chombo hicho kinaunga mkono jitihada za kuendeleza uhusiano ujirani mwema baina ya mataifa.

Katibu Mkuu amesema ni matumaini  yake kuwa hatua hiyo ya kihistoria itanufaisha wananchi wa pande zote mbili ambazo ni Marekani na Cuba.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter