Skip to main content

WHO, WMO zatoa muongozo kuhusu athari za kuongezeka kwa joto

WHO, WMO zatoa muongozo kuhusu athari za kuongezeka kwa joto

Shirika la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na lile la hali ya hewa WMO yametoa muongozo kuhusu joto na mfumo wa afya ukiangazia hatari za kiafya zinazosababishwa na mawimbi ya joto ambayo yanaongezeka ikiwa ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi. Joshua Mmali na maelezo kamili.

(TAARIFA YA JOSHUA)

Muongozo huo unaeleza kuwa mawimbi ya joto ni janga la asili ambalo linahitaji kushughulikiwa ipasavyo kabla yua kuleta madhara makubwa kama ilivyotokea katika baadhi ya sehumu duniani ikiwamo India na barani Ulaya ambapo watu wamekufa kutokana na fukuto linalosababishwa na joto kali.

Serikali na hata jamii kwa ujumla inapaswa kuchukua hatua anuai dhidi ya mawimbi makali ya jotyo na athari zake ambapo mashirika hayo yanaeleza kuwa katika kipindi cha miaka 50 iliyopita joto nyakati za mchana na usiku na mawimbi ya joto yameongezeka duniani.

Clare Nullis ni msemaji wa shirika la kimataifa la hali ya hewa WMO

(SAUTI CLARE)

‘Wakati mwingine ni hatua rahisi tu kwa mfano kuwashauri watu kukaa ndani kuanzia saa nane mchana hadi saa moja jioni au kunywa maji mengi. Kwahiyo kuna hatua rahisi ambazo twaweza kuzichukua na zile za garama lakini inahitaji uratibu wa pamoja kati ya mamlaka za hali ya hewa, serikali na sekta ya afya.’’