Harakati za kukwamua bonde la Mto Kagera zaleta nuru:

Harakati za kukwamua bonde la Mto Kagera zaleta nuru:

Mustakbali wa bonde la mto Kagera ambao unatiririka katika nchi nne za ukanda wa maziwa makuu barani Afrika umekuwa mashakani kwa muda mrefu kutokana na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali zake. Wakati wa nchi hizo ambazo ni Rwanda, Burundi, Tanzania na Uganda wamekuwa wakivua samaki, wakilima au hata kulisha mifugo yao bila kufahamu kuwa matumizi yasiyo endelevu yanahatarisha siyo tu vipato vyao bali pia uhai wao. Hata hivyo sasa nuru imeingia kwani shirika la chakula na kilimo duniani, FAO  linatekeleza mradi katika nchi hizo wenye lengo la kuboresha udongo kwa kutambua kuwa matumizi bora ya ardhi, yataimarisha rutuba ya udongo na kuinua kiwango cha mazao na pia kuhifadhi mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho. Je nini kinafanyika na manufaa ni yapi? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.