Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CUBA yatokomeza maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa Mtoto

CUBA yatokomeza maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa Mtoto

Leo Cuba imetangazwa rasmi kuwa nchi ya kwanza duniani kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi na kaswende kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Shirika la Afya duniani WHO limetangaza hatua hiyo kupitia taarifa iliyotolewa leo, likisema kwamba ni mafanikio makubwa katika kupambana na ukimwi na magonjwa ya zinaa.

Mafanikio yaliyopatikana Cuba yanatokana na mradi wa huduma za afya kwa wote, uliloanzishwa mwaka 2010 kwenye ukanda mzima wa ukanda wa Amerika. Kupitia mradi huo, wanawake wajawazito na wenzi wao wamepatiwa huduma za vipimo, matibabu ya ARV, uzazi kwa upasuaji na maziwa mbadala kwa watoto.

Takwimu za WHO zinaonyesha kwamba kila mwaka, wanawake milioni Moja nukta Nne wenye virusi vya ukimwi wanapata ujauzito, asilimia 15 hadi 45 wakiwa hatarini kuambukiza watoto wao iwapo hawatapata matibabu.

WHO imeeleza kuwa hatari hiyo inapungua hadi asilimia Moja tu iwapo mwanamke na mtoto wanapatiwa matibabu yanayostahili.