Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambuli dhidi ya majengo ya UM Yemen

Ban alaani mashambuli dhidi ya majengo ya UM Yemen

Katibu Mkuu amelaani mashambulizi ya anga katika ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Yemen mnamo Juni 28 yaliyosababisha uharibufu mkubwa katika ofisi ya shirika la UM la mpango wa maendeleo UNDP na kujeruhi mlinzi.

Taarifa kupitia kwa msemaji wa Katibu Mkuu inamkariri Ban akisema kuwa sheria za kimataifa zianataka ulinzi kwa pande zote za raia na mali zao ikiwamo zile za UM. Amesema kutodhuru majengo ya UM na kazi muhimu za wafanyakazi wa umoja huo lazima viheshimiwe wakati wote.

Katibu Mkuu ametaka uchunguzi wa kina kuhusu tuko hilo na ikiwa mtu yeyote atabainika kuhusika awajibishwe. Ameongeza kuwa hakikisho la uwajibikaji ni muhimu katika kuzuia matukio kama hayo.

Amesema shambulio hilo linasisitiza umuhimu wa pande kinzani kukomesha machafuko na kurejea katika meza ya mazungumzo kama njia pekee ya kufikia amani ya kudumu nchini Yemen.