Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ngoma ya Isukuti ni moja ya tamaduni zilizopendekezwa kulindwa na UNESCO

Ngoma ya Isukuti ni moja ya tamaduni zilizopendekezwa kulindwa na UNESCO

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa linahimiza ulinzi wa tamaduni mbali mbali kote ulimwenguni, hususan ambazo ziko katika hatari ya kupotea au kuharibiwa.

Miongoni mwa tamaduni hizo ni ngoma ya Isukuti ambayo ni muhimu katika kabila la wa Waluhya la kutoka Magharibi mwa Kenya. Je ngoma hii ina nafasi gani katika jamii mbali mbali? Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.