Skip to main content

UNWTO yalaani vikali shambulizi la Sousse, Tunisia

UNWTO yalaani vikali shambulizi la Sousse, Tunisia

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Utalii Duniani, WTO, limelaani vikali mashambulizi yaliyotekelezwa leo katika miji ya Sousse Tunisia, Lyon Ufaransa na mji wa Kuwait nchini Kuwait.

Katibu Mkuu wa WTO, Taleb Rifai, amesema kwamba mashambulizi hayo yanabainisha kuwa ulimwengu unakabiliwa na tishio la kimataifa.

Bwana Rifai ametuma risala za rambi rambi kwa familia za wahanga, na kukariri uungaji mkono wake kikamilifu kwa watu na serikali ya Tunisia, ambayo amesema imekuwa ikipigana kwa muda mrefu dhidi ya uhalifu huo ili kurejesha imani katika sekta yake ya utalii.

Amesema mashambulio hayo ni mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya vitega uchumi vya watu wa Tunisia. Amesema utalii ni tegemeo la uchumi wa nchi hiyo, na kwa hiyo WTO itaendelea kuunga mkono sekta hiyo ukwamuaji wa sekta hiyo muhimu kwa ajili ya mustakhbali wa watu wa Tunisia.