Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani

Maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani

Wakimbizi ni watu wa kawaida, kama mimi na wewe. Hii ni sehemu ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon aliuotoa wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya wakimbizi ambayo huadhimishwa Julai 20 kila mwaka. Bwana Ban ametaka kote duniani watu kuwavumilia kwa kuwaonyesha utu na kufungua mioyo kwa ajili ya wakimbizi.

Siku hii adhimu ilipitishwa na baraza kuu la UM mnamo Desemba nne mwaka 2000 kupitia azimio nambari 55/6 ambapo azimio hili lilibainisha kuwa mwaka 2001 ikiwa ni miaka 50 ya mkataba kuhusu hadhi za wakimbizi na kwamba uliokuwa muungano wa nchi za  Afriaka wakati huo ukiitwa OAU sasa AU ulikubali kuwa siku ya kimataifa ya wakimbizi iende sambamba na siku ya wakimbizi kwa bara la Afrika na hivyo kufanyaika pamoja Julai 20.

Je hali sasa ikoje na maadhimisho yaliangazia nini? Ungana na Amina Hasan katika makala hii.