Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya kigaidi Tunisia, Kuwait na Ufaransa

Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya kigaidi Tunisia, Kuwait na Ufaransa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea leo nchini Tunisia, Ufaransa na Kuwait na kusababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu na majeruhi.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Katibu Mkuu amenukuliwa akisema wale waliotekeleza uhalifu huo wa kusikitisha wanapaswa kupelekwa mbele ya sheria.

Aidha Bwana Ban amesema kwamba mashambulizi hayo yataongeza utashi wa jamii ya kimataifa wa kupambana na ugaidi, na msimamo wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia walioathirika na janga la kigaidi, ambalo lengo lake ni kuharibu utamaduni na maendeleo ya binadamu.

Halikadhalika, Katibu Mkuu ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga, akikariri mshikamano wake na raia wa Tunisia, Kuwait na Ufaransa.

Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa ametoa taarifa kulaani mashambulio hayo huku akituma rambirambi kwa wafiwa na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi na kutaka nchi wanachama kuimarisha jitihada za kushughulikia misimamo mikali inayochochea ghasia