Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya ngome ya AMISOM

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya ngome ya AMISOM

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Somalia,  Nicholas Kay, amelaani vikali shambulio lililofanywa leo na kundi la Al Shabaab dhidi ya ngome ya vikosi vya Muungano wa Afrika, AMISOM huko Leego. Ngome hiyo ilikuwa chini ya vikosi vya Burundi.

Kay ametuma rambi rambi zake kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika shambulio hilo, na kwa serikali na watu wa Burundi.

Amesema walinda amani hao jasiri wametoa maisha yao katika juhudi zinazoendelea za kuleta amani ya kudumu na ustawi nchini Somalia.

Ameongeza Umoja wa Mataifa hautafifia katika kuunga mkono watu wa Somalia, na katika kushikamana na Muungano wa Afrika na vikosi vya usalama vya Somalia katika juhudi za kushinda al-shabaab na kujenga amani na ustawi nchini humo.