Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi waongezeka nchi rajani wakihofia uchaguzi Burundi: UNHCR

Wakimbizi waongezeka nchi rajani wakihofia uchaguzi Burundi: UNHCR

Hofu ya machafuko imesababisha ongezeko kubwa la wakimbizi kutoka Burundi ambao wanamiminika nchi jirani ikiwamo Tanzania, Rwanda, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia limesema shirika la Umoja wa Mataifa la  kuhudumia wakimbizi UNHCR.Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa UNHCR  Adrian Edwards amesema uchaguzi wa wabunge nchini Burundi mnamo Juni 29 umesababaisha raia wengi kutoka nchini humo wanaohofia  mashambulizi ya magurunedi,  ukamatwaji hovyo na kwa ujumla ukosefu wa utulivu nchini Burundi kusaka hifadhi nchi jirani huku idadi kubwa ikielekea Tanzania.

(SAUTI ADRIAN)

‘‘Nchini Tanzania wakimbizi wanaendelea kuwasIli katika kiwango cha 200 hadi 300 kwa siku. Wanasafirishwa hadi kambi ya Nyarugusu ambayo inaelemewa. Nchini Rwanda idadi ya  wanaowasili imeongezeka kwa kipindi cha  siku chache zilizopita , Nchini DRC jimboni Kivu kusini wakimbizi walikuwa wanaishi na wenyeji wakiwemo wakimbizi ambao walikimbia Burundii miaka mingi iliyopita."

Hata hivyo amesema idaidi kamili ya raia waliokimbia nchi haijulikani kwani inadaiwa wengi hawajasajiliwa kama wakimbizi katika nchi walizofikia.