Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asisitiza amani na kuahirishwa uchaguzi Burundi

Ban asisitiza amani na kuahirishwa uchaguzi Burundi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anafuatilia kwa umakini hali nchini Burundi na kupongeza juhudi za upatanishi zinazofanywa na timu ya pamoja  ya kimataifa inayohusisha jumuiya ya Afrika Mashariki , muungano wa Afrika, kongamano la ukanda wa maziwa makuu na Umoja wa Mataifa katika kusaidia pande nchini Burundi kufikia makubaliano na kuhakikisha amani na uchaguzi huru. Taarifa ya Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu Bwana Ban akisema kuwa anasikitishwa na kuzorota kwa hali ya kiusalama na kisisasa nchini Burundi na kutaka mamlaka nchini humo kuzingatia kwa umakini mkubwa pendekezo la kuahirisha uchaguzi toka jumuiya ya kimataifa.

Amesema hilo litawezesha mazingira bora zaidi na ya uchaguzi wa  amani na uwazi kulingana na maamuzi ya hivi karibuni ya baraza la usalama la  Muungano wa Afrika na mkutano wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu amesisitiza wito wake kwa wadau wa siasa nchini Burundi kutumia njia ya majadiliano katika kutafuta suluhu kwa maslahi ya watu wa Burundi kwa ajili ya amani na usalama wa taifa.