Dunia ni lazima iongeze kasi ya kupambana na HIV au kuepuka maambukizi zaidi

25 Juni 2015

Ripoti mpya ya Shirika linalohusika na masuala ya Ukimwi katika Umoja wa Mataifa, UNAIDS na Kamisheni ya Lancet, imesema kuwa nchi ambazo zimeathiriwa zaidi na HIV ni lazima ziangazie kuzuia maambukizi mapya na kupanua upatikanaji wa matibabu ya dawa za ARV, la sivyo zitakuwa katika hatari ya maambukizi na vifo Ukimwi kutokana na Ukimwi kuliko miaka mitano ilyopita.Taarifa kamilia na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Ripoti hiyo iitwayo, ‘Kushinda Ukimwi- kuendeleza afya duniani’ inaonyesha kuwa, ingawa hatua zimepigwa katika kuongeza idadi ya watu wanaotibiwa kote duniani dhidi ya HIV, kiwango cha maambukizi mapya ya HIV hakishuki haraka ipasavyo.

Ripoti imesema kuwa maambukizi hayo, pamoja na kuongezeka idadi ya watu katika nchi zilizoathiriwa, kunaongeza idadi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi, na ambao watahitaji matibabu ya ARV ili waendelee kuishi.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé, amesema kuwa sasa ndio wakati wa kuchukua hatua, na miaka mitano ijayo itatoa fursa ya kuongeza kasi ya jitihada, ili kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030, na la sivyo, athari zake kwa binadamu na kwa uchumi zitakuwa ni janga.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter