Skip to main content

Baada ya mafanikio Afrika Mashariki, ubia wa FAO na Rabobank kupanua wigo

Baada ya mafanikio Afrika Mashariki, ubia wa FAO na Rabobank kupanua wigo

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO na taasisi ya Uholanzi ya Rabbobank wanaimarisha ushirikiano wao baada ya ubia wao wa miaka miwili kuleta mafanikio makubwa huko Kenya, Ethiopia na Tanzania.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva wakati wa mkutano wa foodFIRST unaofanyika Utretch, Uholanzi akisema kupitia ubia huo, vipato vya wakulima wadogo kwenye maeneo hayo vimeongezeka, wamepata pembejeo za kilimo na hata  kuzalisha kwa tija mazao ya chakula.

Bwana da Silva amesema kutokana na hali hiyo ubia huo sasa utaongezeka hadi nchi za Latin Amerika, Asia na kwingineko barani Afrika na hivyo kusaidia kutokomeza njaa na kupunguza umaskini kwa kuwa hakuna taasisi moja inayoweza kufikia lengo hilo peke  yake.

Nchini Tanzania mradi huo umewezesha wakulima wa mpunga wilayani Morogoro kupata huduma za kifedha ilihali huko Kenya wakulima wanapatiwa huduma za kuwawezesha kupata mbegu bora.