Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaharia ni taaluma, vijana changamkieni kwani wanahitajika:IMO

Ubaharia ni taaluma, vijana changamkieni kwani wanahitajika:IMO

Ikiwa leo ni siku ya mabaharia duniani katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa  vijana kujiunga na taaluma hiyo akisema kadri dunia inavyosonga mbele, shughuli za usafirishaji bidhaa zinaongezeka, lakini mabaharia wanapungua na hilo ni jambo linalotia hofu.

Katika ujumbe wake amesema ubaharia siyo tu unatoa ajira ya kuboresha maisha bali pia unawezesha kusafiri, kujifunza na kuinua uchumi wa nchi kwa kusafirisha bidhaa.

Irene Waite ambaye ni afisa kutoka idara ya mikutano ya shirika la kimataifa la masuala ya bahari, IMO anafafanua kwa kina lengo la ujumbe wa mwaka huu ambao ni Taaluma baharini.

(Sauti ya Irene)

Amesema IMO inachukua hatua kwa kuzindua mpango wa kuwa na mabalozi wa masuala ya ubaharia ambapo..

(Sauti ya Irene)

Mabaharia wakiwa kwenye meli hufanya shughuli mbali mbali ikiwemo unahodha wa meli, uhandisi na kuhudumia abiria.