Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini yatangaza mlipuko wa kipindupindu

Sudan Kusini yatangaza mlipuko wa kipindupindu

Wizara ya Afya ya Sudan Kusini imetangaza mlipuko wa kipindupindu katika kata ya Juba nchini humo, kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu, OCHA.

Kwa ujumla, visa 170 vinavyodhaniwa kuwa ni vya kipindupindu vimeripotiwa, vikiwemo vifo 18.

Vituo vya matibabu ya kipindupindu vimewekwa kwenye hospitali ya mafunzo ya Juma na kwenye kliniki ya Shirika la kimataifa la matibabu (IMC) katika maeneo ya Umoja wa Mataifa ya ulinzi wa raia, ili kudhibiti visa vinavyodhaniwa kuwa ni kipundupindu.