Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kando ya kuwepesisha mwili na akili, yoga yachangia amani ya kimataifa

Kando ya kuwepesisha mwili na akili, yoga yachangia amani ya kimataifa

Mwaka huu wa 2015, Umoja wa Mataifa umedhihirisha tarehe 21 Juni kama siku ya kimataifa ya yoga, kutokana na manufaa ya mazoezi hayo kwa afya ya akili na mwili wa binadamu, na pia kwa maadili yake na mchango wake katika kuheshimiana na kukuza amani endelevu duniani.

Mazoezi hayo marufuu nchini India tangu maelfu ya miaka iliyopita sasa yanapendwa duniani kote.

Mjini New York Marekani, viongozi wa Umoja wa Mataifa walikusanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ili kushiriki kwenye somo moja la yoga lililoandaliwa na Ujumbe wa Kudumu wa India kwenye Umoja wa Mataifa. Priscilla Lecomte anakusimulia zaidi kwenye makala hii…