Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makubaliano ya amani yasikwepeshe uwajibikaji:OHCHR

Makubaliano ya amani yasikwepeshe uwajibikaji:OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, imesema ni matumaini yake kuwa makubaliano ya amani yaliyotiwa saini huko Mali, mwishoni mwa wiki hayafungua njia ya ukwepaji sheria kwa wahusika wa makosa ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa ofisi hiyo Ravina Shamdasani alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi baada ya waasi wa kikundi cha Azawad kutia saini makubaliano hayo.

(Sauti ya Ravina)

“Tunakaribisha kigezo kwenye makubaliano ya kwamba sheria ya msamaha haitapitishwa kwa makosa makubwa ya ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Sheria za kimataifa na sera za Umoja wa Mataifa ziko bayana kuwa misamaha haikubaliki iwapo inaepusha mashtaka ya makosa ya uhalifu wa kivita, uhalifu wa kibinadamu, mauaji ya kimbari na ukiukaji wa haki za binadamu.”

Amesema wameunga pia mkono pendekezo la kuanzisha tume ya kimataifa ya kuchunguza madai ya makosa ya aina hiyo akisema ili amani iwe endelevu ni lazima haki na uwajibikaji upatiwe kipaumbele.