Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utajiri wa watu 80 tajiri zaidi duniani ni sawa na maskini Bilioni 3.5 duniani kote

Utajiri wa watu 80 tajiri zaidi duniani ni sawa na maskini Bilioni 3.5 duniani kote

Pengo la walio nacho na wasio nacho linazidi kukua kila uchao na hivyo ni lazima serikali zijiulize kulikoni hali hiyo inazidi kuota mizizi na kutumbukiza nyongo haki za msingi za binadamu.

Ni kauli aliyotoa Phillip Aston,  mtaalamu maalum wa haki za binadamu kuhusu umaskini wakati wa mjadala wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu ufukara uliofanyika leo huko Geneva, Uswisi.

Amesema cha ajabu licha ya kwamba Baraza hilo limekuwa likitoa mapendekezo kubadili mwelekeo lakini bado pengo ni kubwa kwani utajiri wa watu 80 tajiri zaidi duniani ni sawa na mali za watu Bilioni Tatu na nusu maskini zaidi duniani, hivyo amesema baraza liache maneno matupu na badala yake..

(Sauti ya Phillip)

Hatua zetu zinapaswa kushinikizwa sio tu na vitisho vikubwa kwa haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni, bali pia kwa ukweli kwamba upatikanaji wa haki za kiraia na kisiasa  unakwamishwa na pengo kubwa sana la ukosefu wa usawa.”