Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuhuma za uhalifu wa kivita kwenye mashambulizi Gaza ni dhahiri: Ripoti

Tuhuma za uhalifu wa kivita kwenye mashambulizi Gaza ni dhahiri: Ripoti

Kamisheni huru iliyoundwa kuchunguza mzozo wa Gaza wa mwaka 2014 imebaini tuhuma dhahiri zinazoweza kusababisha janga lililotokea wakati huo na kusababisha vifo vya maelfu ya watu kuwa wa kivita.

Hiyo ni kwa mujibu wa mwenyekiti wake Jaji Mary McGowan alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi leo wakati akiwasilisha ripoti hiyo akisema vitendo hivyo vilitekelezwa na Israel na vikundi vilivyojihami vya kipalestina.

Amesema uharibifu uliofanyika na machungu yaliyotoka na mapigano hayo yaliyodumu kwa siku 51 utadumu vizazi na vizazi na hivyo wamependekeza..

(Sauti ya Jaji Mary)

“Tunatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchagiza na kuimarisha harakati za kisheria na kanuni za kudhibiti matumizi ya vilipuzi kwenye maeneo ya raia na yale yenye idadi kubwa ya watu kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa raia wakati wa chuki na mapigano.”

Mwenyekiti huyo na mjumbe wake Doudou Diene wamesema hawakupata kibali kwenda Israel na maeneo ya kipalestina yanayoshikiliwa kwa hiyo uchunguzi walifanya kwa mahojiano ya njia ya Sykpe, Video na simu.

Kamisheni hiyo itawasilisha rasmi ripoti yake mbele ya Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa tarehe 29 mwezi huu huko Geneva.