Skip to main content

UNRWA yazindua kampeni ya watoto sambamba na mwezi wa Ramadan

UNRWA yazindua kampeni ya watoto sambamba na mwezi wa Ramadan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA leo limezindua kampeni ya usaidizi kwa watoto wa Gaza  iitwayo #SOS4Gaza ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kuanza kwa mfungo wa mwezi wa Ramadan .

Kwa mujibu wa taarifa ya UNRWA kampeni hii inatumia filamu  inayoonyesha watoto saba wakitoa ujumbe wakuelezea matumaini yao na ndoto katika chupa walizozituma baharini ambapo ujumbe ni namna watoto wa Gaza walivyorushwa nyuma kutokana na machafuko mwaka jana.

Kwa mujibu wa Kamishna  mkuu wa UNRWA Pierre Krähenbühl licha ya changmoto hizo watoto Gaza wana ndoto na wanahitaji mustakabli mwema kama watoto wengine na akasema kuwa ni jambo jema kuona  watoto walioshirikishwa katika filamu hiyo ambao ni takribani 950,000 wamekuwa katika umasikini na mizozo lakini hawajapoteza matumaini.

Kampeni inaongozwa na balozi mwema wa UNRWA ukanda huo  na anayehusika na vijana na nguli  kutoka Uarabuni Mohammad Assaf.