Skip to main content

Mjumbe wa UM alaani shambulizi dhidi ya gari la raia wa Israel

Mjumbe wa UM alaani shambulizi dhidi ya gari la raia wa Israel

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mchakato wa Amani Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov, amelaani shambulizi la risasi dhidi ya gari la raia wa Israel katika maeneo yaliyokaliwa Ukingo wa Magharibi, ambalo limesababisha kifo cha mtu mmoja na kumjeruhi vibaya mwingine.

Amesema kwenye siku hii ya pili ya Ramadan na mwanzoni mwa Sabato, anatoa wito kwa pande zote kujizuia kabisa, ili kuendeleza utulivu, na kuwafikisha wahalifu mbele ya mkono wa sheria.