Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kukabiliana na Kifua Kikuu sugu nchini Tanzania

Harakati za kukabiliana na Kifua Kikuu sugu nchini Tanzania

Kifua Kikuu sugu, MDR-TB ugonjwa ambao unaendelea kuwa mwiba kwa watu 480,000 duniani kote, Tanzania ikiwa ni miongoni mwao. Shirika la afya duniani, WHO linasema kuwa MDR-TB ni ile ambayo ni sugu kiasi kwamba inagoma kutibika kwa dawa aina za isoniazid na rifampicin, ambazo yaelezwa ni tiba thabiti zaidi dhidi ya Kifua Kikuu. Sababu kuu za usugu ni matumizi mabaya ya dawa hizo wakati wa matibabu, mathalani wagonjwa kuruka siku za kupatiwa tiba au ubora duni wa dawa zenyewe. Wagonjwa wanahaha, siyo tu kwenye kusaka tiba bali pia yale yatokanayo na tiba, mfano lishe kwani yasemekana tiba bora ni ile iendayo sanjari na lishe bora. Je hali ya matibabu nchini Tanzania ikoje? Tuungane na Grace Kaneiya.