Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saksafoni yapunguza machungu ya ukimbizini

Saksafoni yapunguza machungu ya ukimbizini

Kuelekea siku ya wakimbizi duniani tarehe 20 Juni mwaka huu wa 2015, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeweka bayana simulizi za wakimbizi kutoka maeneo mbali mbali duniani ambao kutwa kucha wanasaka maisha bora kule walikokimbilia huku taswira ya maisha ya nyumbani ikiendelea kusalia katika fikra zao. Miongoni mwa simulizi hizo ni ile ya Nader, mkimbizi kutoka Syria ambaye sasa anaishi Thailand.

Kiburudisho chake yeye na familia yake ni ala ya muziki ambayo awali akiwa nyumbani Syria ilikuwa ni njia ya kujipatia kipato, lakini sasa ugenini, hana la kufanya. Hata hivyo nuru imebisha hodi. Je ni nini kimefanyika? Ungana na Assumpta Massoi katika makala hii.