Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yasikitishwa na shambulio la grunedi katika shule Bujumbura

UNICEF yasikitishwa na shambulio la grunedi katika shule Bujumbura

Shirika la kuhudumia watoto UNICEF, limesema limesikitishwa na shambulio la gruneti katika shule mjini Bujumbura, Burundi, ambalo limemjeruhi kijana mwenye umri wa miaka 15. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa UNICEF Christophe Boulierac amesema wakati huu wa machafuko nchini Burundi, watoto wanaendelea kuuawa, kutiwa vizuizini, na kuwa katika hali ya hatari mno, akitoa wito.

"UNICEF inakariri kuwa watoto wana haki ya kulindwa katika hali kama hizo na kamwe wasilengwe, na kwamba shule zinapaswa kuheshimiwa kama sehemu ya amani na maficho salama kwa watoto".

Wakati huo huo  Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukuzaji wa ukweli, haki na ulipaji fidia Pablo de Greiff, amesema kwenye taarifa iliyotolewa leo kwamba uchaguzi huru hauwezi kufanyika nchini Burundi kwa sababu ya mazingira yaliyopo sasa hivi ya ukatili, mateso na vitisho, akilaani utamaduni wa ukwepaji sheria nchini humo na akimulika hatari za kuenea kwa mzozo wa kikabila.