Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu lamulika ukatili wa majumbani dhidi ya wanawake

Baraza la Haki za Binadamu lamulika ukatili wa majumbani dhidi ya wanawake

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo limekuwa na mjadala wa siku nzima kuhusu haki za binadamu za wanawake, likimulika hasa kuzuia na kutokomeza ukatili majumbani dhidi ya wanawake na wasichana.

Rais wa Baraza hilo, Joachim Rüecker, amesema hatua zimepigwa katika miaka ishirini iliyopita, kwani sasa ukatili dhidi ya wanawake sasa ni suala linalomulikwa kimataifa, na siyo tena suala la faragha. Licha ya hayo, amesema ukatili dhidi ya wanawake bado umeenea, serikali hazijalikubali suala hilo kama suala la haki za binadamu.

Naye Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Flavia Pansieri, amesema takwimu za ukatili majumbani dhidi ya wanawake zinatia shaka, kwani mmoja kati ya wanawake watatu duniani anakumbana na aina fulani ya ukatili katika uhai wake.

Kwenye kitovu cha ukatili huu ni imani kuwa wanaume wana mamlaka juu ya wanawake na haki ya kudhibiti tabia zao na kulinda hadhi yao. Njia ya kukabiliana na athari za ukatili na hatua za kiserikali ni muhimu, kuangazia sheria zenye kubagua ni muhimu, kuhakikisha  kuwajibisha wanaokosa na kuwalipa fidia waathirika. Hii inahitaji hatua ya kuimarisha mashitaka ambayo itabadili mtazamo wa jamii wa tabia ipi ilo haki na ipi inayokubalika."