Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola bilioni moja yahitajika kunusuru waathiriwa wa machafuko Yemen: OCHA

Dola bilioni moja yahitajika kunusuru waathiriwa wa machafuko Yemen: OCHA

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa wito wa changizo la dola bilioni moja nukta sita kusaidia watu milioni 11.7 walioathiriwa na mgogoro unaondelea nchini Yemen huku kukiwa na upungufu wa dola bilioni moja nukta nne hadi kufikia mwisho wa mwaka huu.

Kwa mujibu wa mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA Stephen O’Brien wakati wa uzinduzi wa changizo hilo mjini Geneva  Uswis, raia nchini humo wanahaha kulisha familia zao huku huduma muhimu za kijamii zikiwa zimedumaa.

Amesema mamilioni ya watu hawapati maji safi, huduma za kujisafi na huduma za afya na kuongeza kuwa jamii hiyo inakabiliwa na magonjwa kama vile homa ya dengue na malaria huku  huduma dhidi ya athari za kisaikolojia ikiwamo kiwewe zikiwa zikiyoyoma.

Mkuu huyo wa OCHA amesisistiza umuhimu wa changizo hilo akisema  maelfu ya watu wameuwawa na kujerughiwa na mashambulizi ya anga na ardhini katiak meizi mitatu iliyopita. Watu milioni moja wamekimbia Yemen na asilimai 80 ya raia hao wanahitaji msaada wa kibinadamu.