Matumaini mapya kwa wahamiaji na wakimbizi walionusuriwa Mediterenia

18 Juni 2015

Kufikia mwezi Juni, idadi ya wakimbizi na wahamiaji waliowasili Ulaya kupitia Bahari ya Mediterenia ni 112,000. Mnamo Jumanne, meli ya wanamaji wa Ireland iliwanusuru watu 400, na kuwapeleka kusini mwa Italia, ambako sasa wanapata usaidizi. Miongoni mwao, walikuwamo watoto na wanawake waja wazito.Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, wengi wa wahamiaji na wakimbizi hao walitoka kusini mwa jangwa la Sahara. Baadhi yao walikuwa wanatafakari kuhusu hatma yao, huku wengine wakiwa hawajui hatari ambazo wangekumbana nazo baharini. Ungana basi na Joshua Mmali, akisimulia kuhusu hatma yao katika Makala hii

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter