Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa sheria unaoshindwa kutendea haki watoto unaifeli jamii nzima:mtalaam wa UM

Mfumo wa sheria unaoshindwa kutendea haki watoto unaifeli jamii nzima:mtalaam wa UM

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na mawakili, Gabriela Knaul, amesema kwamba jinsi watoto wanavyotendewa haki mahakamani haikubaliki.

Bi Knaul amesema hayo leo akipeleka matokeo ya ripoti yake mbele ya Baraza la Haki za Binadamu, mjini Geneva Uswisi. Ameongeza kuwa kila siku watoto wanateseka kwa sababu mifumo ya sheria inakiuka haki zao za msingi.

Ameomba nchi zitengeneze mifumo ya sheria inayoheshimu na kutunza haki za watoto na kutimiza mahitaji yao kama watoto, akipendekeza mifumo mbadala ianzishwe ili kuzuia watoto wasipitie kwenye mahakama ya kawaida.

Hatimaye Bi Knaul amesema ni wajibu wa majaji na wawakili kuleta mabadiliko kwenye mifumo ya sheria ili kuimarisha maisha ya watoto.