WHO yahimiza tahadhari zaidi dhidi ya homa ya MERS

18 Juni 2015

Shirika la Afya Duniani, WHO, limetoa wito wa kuwepo tahadhari zaidi dhidi ya homa ya kirusi cha corona, kufuatia serikali ya Thailand kuthibitisha kuwa msafiri mmoja aliyewasili nchini humo kutoka Mashariki ya Kati amepatikana kuwa na homa hiyo. Hicho ndicho kisa cha kwanza cha homa ya corona kwenye ukanada wa Kusini Mashariki mwa Asia.

Mkurugenzi wa WHO katika ukanda wa Kusini Mashariki mwa Asia, Dkt. Poonam Khetrapal Singh, amesema mifumo thabiti ya afya inayochukua hatua kali za kuzuia maambukizi inaweza kuwa ndiyo njia bora ya kuzuia kuenea kwa kirusi hicho na kuwalinda wahudumu wa afya na watu wengine.

Ametoa wito kwa nchi katika ukanda huo kuongeza uangalifu kuhusu wagonjwa wanaoweza kueneza maambukizi, kuangazia upimaji wa mapema na kuongeza shughuli za kuzuia maambukizi katika vituo vya afya.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter