Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji katika bima ni muhimu katika kukabliana na majanga: Ban

Uwekezaji katika bima ni muhimu katika kukabliana na majanga: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon amesema jamii ya bima duniani ni muhimu katika mustakabali endelevu wa dunia kwani ni uwekezaji muhimu.

Katika hotuba yake wakati wa mkutano wa kimataifa wa jamii ya mashirika ya bima hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Ban amesema bima ni suala lisilokwepeka kupunguza majanga huku akiangazia zaidi janga linaloikumba dunia la mabadiliko ya tabianchi.Amesema ni wakati wa kuchukua hatua ya kimataifa katika kupunguza majanga ambazo sio tu haziathiri tabia nchi bali pia zitakuwa fursa na usalama kwa maendeleo endelevu.

Amewakumbusha washiriki wa mkutano huo kuwa bima ina mchango mkubwa katika kuelekea mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwa kusema kuwa uwekezaji katika bima lazima uhimizwe kwa kutikiza ahadi ambazo jamii ya bima iliahidi katika makabiliano hayo.