Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko wa MERS-Corona bado haujafikiwa kiwango cha janga:WHO

Mlipuko wa MERS-Corona bado haujafikiwa kiwango cha janga:WHO

Shirika la afya duniani, WHO limesema bado kirusi cha Corona kilichosababisha vifo vya watu 19 huko barani Korea Kusini hakijaweza kufikia kiwango cha kuleta udharura duniani licha ya kwamba kinaweza kusababisha maambukizi zaidi.

Hiyo ni kwa mujibu wa kamati ya dharura ya WHO iliyofuatilia kirusi hicho kilicholeta madhila Korea Kusini na kwa kiasi nchini China.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Dokta Keiji Fukuda amesema mlipuko wa ugonjwa huo ni kiashiria cha kuiweka dunia katika tahadhari kubwa lakini kuendelea kupungua kwa maambukizi mapya ni dalili kuwa jitihada za kudhibiti kuenea kwake zinafanya kazi, lakini.

(Sauti ya Fukuda)

"Ni dhahiri kabisa ni vyema kuendeleza usimamizi wa hali ya ju na ufuatiliaji hadi tutakapothibitisha kuwa mlipuko huu umetokomea."

Hadi leo hakuna tiba dhidi ya kirusi hicho kilichokumba watu 162 huko Korea Kusini na dalili za ugonjwa wake zinafanana na mafua.