Skip to main content

Ulinzi wa raia changamoto kwa operesheni za amani: Baraza la Usalama

Ulinzi wa raia changamoto kwa operesheni za amani: Baraza la Usalama

Baraza la Usalama limekutana leo mjini New York, Marekani, kwa ajili ya kutathmini operesheni zote za ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa, wakuu wa vikosi vya kulinda amani wakitoa ushahidi wao kuhusu maswala yanayogusa ujumbe za Umoja wa Mataifa siku hizi, yakiwemo ulinzi wa raia. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Kuhusu ulinzi wa raia, Yohannes Gebremeskel Tesfamariam, mkuu wa kikosi cha walinda amani wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS ameeeleza kwamba walinda amani wao wanateseka katika jitihada zao za kulinda raia, pande za mzozo zikiwazuia kufikia wanaohitaji, na kambi za UNMISS zikilengwa na makombora.

Aidha amesema kuwa lengo la UNMISS sasa ni kulinda usalama wa raia kwenye makazi yao, ili waweze kuendelea na shughuli zao kama mfano kilimo, kwa sababu kuwepo kwa wakimbizi wapatao 140,000 kwenye kambi za UNMISS si jambo endelevu.

“ Baadhi ya wakimbizi wa ndani wanabaki kwenye kambi kwa muda mrefu kwa sababu huduma zinatolewa. Tunapaswa kutathmini uendelevu wa utaratibu huo. Bila amani ya kudumu nchini humo, tunapaswa kutathmini ni kwa muda gani Ujumbe unapaswa na unaweza kuwapa hifadhi watu wanaoishi sasa hivi kwenye kambi za ulinzi.