Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwaleta Geneva wajumbe wa pande kinzani Yemen ni hatua adhimu- UM

Kuwaleta Geneva wajumbe wa pande kinzani Yemen ni hatua adhimu- UM

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen, Ould Cheikh Ahmed, amesema kuwa baada ya kuepukana na changamoto kubwa, kuweza kuwaleta wajumbe wa pande zote kinzani nchini Yemen mjini Geneva ni hatua ya ufanisi mkubwa, na ambayo inapaswa kupewa uzito.

Amesema kufika kwa wajumbe hao Geneva ni hatua muhimu ya kuanza kuelekea kurejelea mchakatao wa kisiasa na kwamba..

"Mashauriano ni hatua ya kwanza ya mchakato wa kuanzisha mapendekezo kwa pande za Yemen juu ya jinsi ya kuboresha hali ya sasa, kurejesha utulivu na kumaliza taabu ya wananchi."

Aidha, ameonya kuwa haitakuwa rahisi, lakini akasema lililo muhimu ni kuanza kukabiliana na mzozo wa Yemen kwa njia zote, kwa ari na utashi, na kwamba kazi hiyo inaanza Geneva.

Bwana Ahmed amesema watu wa Yemen na jamii ya kimataifa wanayaona mashauriano ya Geneva kama njia ya amani ya kumaliza mzozo na kulinda mafanikio ya mpito ya Yemen.