Kufunga mipaka ya kimataifa kunawatia nguvu wasafirishaji haramu- Mtaalam wa UM

Kufunga mipaka ya kimataifa kunawatia nguvu wasafirishaji haramu- Mtaalam wa UM

Uwezo wa wahamiaji kufika Ulaya licha ya uwekezaji mkubwa katika kudhibiti mipaka ya kimataifa kunaonyesha kuwa ni vigumu kufunga kabisa mipaka, na kunawawezesha tu wasafirishaji haramu wa watu. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Hayo yamesemwa leo na Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki binadamu za wahamiaji, François Crépeau.  Akiwasilisha ripoti yake ya hivi karibuni zaidi kwa Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Bwana Crépeau amesema Muungano wa Ulaya na nchi wanachama wake ni lazima zitambue kuwa uhamiaji ulio kinyume na taratibu unatokana sera zinazozuia uhamiaji.

Amesema sera kama hizo badala yake hufungua soko la faida kubwa kwa magenge ya wasafirishaji haramu, na kwamba soko hilo lisingalikuwepo bila sera hizo zinazozuia uhamiaji.

“Kwa kuweka vizuizi, tumefungua soko kwa wasafirishaji haramu, na wasafirishaji haramu wanatoa huduma za usafiri ambazo watu hawa wanahitaji. Ni dhahiri kuwa, tusijaribu kuendelea na mikakati na sera za kuzuia uhamiaji. Kwa sababu uzuiaji unazaa masoko haramu.”