Wajumbe zaidi wawasili Geneva katika kusaka amani Yemen

16 Juni 2015

Wajumbe katika mashauriano ya kusaka suluhu ya mgogoro nchini Yemen wakiwamo kundi la Houthi kutoka mji mkuu Sana’a wamewasili mjini Geneva kwa ajili ya mashauriano hayo yanayoyotoa matumaini ya kuhitimisha uhasama na kujenga amani, demokarisa thabiti nchini Yemen.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva Ahmad Fawzi, mratibu wa mazungumzo hayo yaliyoanza jana ambaye ni mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed anatarajiwa kuzungumza na kila upande kwa matumaini ya kuwaleta pamoja wote baadaye.

(SAUTI FAWZI)

‘Wajumbe kutoka Sana’a, wamewasili mapema leo asubuhi, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu atakutana nao leo badae katika hotel yao kujadiliana nao kuhusu muundo wa ujumbe wao na kuhakikisha unaendana na makubaliano ambayo ni saba jumlisha tatu kwa kila ujumbe . Yaani maafisa saba na washauri watatu." 

Hapo jana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon alitaka pande kinzani nchini humo kusitisha mapigano angalau kwa majuma mawili katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter