Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNIDO na China kushirikiana kuimarisha usalama wa chakula na dawa barani Afrika

UNIDO na China kushirikiana kuimarisha usalama wa chakula na dawa barani Afrika

Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) na Mamlaka ya Dawa na Chakula ya China wametangaza leo kuanzisha mradi wa pamoja kuhusu usalama wa chakula na dawa, unaolenga biashara ya madawa na uzalishaji barani Afrika.

Mkurugenzi wa UNIDO Li Yong amesema tayari shirika lake limesaidia zaidi ya kampuni 230 za kuzalisha vyakula barani Afrika na Asia kupata cheti cha kiwango cha kimataifa katika uzalishaji bora, pamoja na maabara 200 kufikia kiwango cha kimataifa katika upimaji wa vyakula.

Bwana Li ameongeza kuwa ushirikiano kati ya China na UNIDO unalenga maeneo mawili ambayo ni usalama wa chakula na viwanda rafiki kwa mazingira.

Tayari baadhi ya viwanda nchini China vimesaidiwa kupata cheti cha kimataifa aina ya ISO 22000, UNIDO ikisema mradi huo umesaidia kukuza biashara nchini humo pamoja na kulinda wateja.