Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio huko N’Djamena, 25 wauawa, Ban alaani vikali

Shambulio huko N’Djamena, 25 wauawa, Ban alaani vikali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la leo huko N’Djamena, Chad lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 25 na makumi kadhaa wamejeruhiwa.

Ban amekaririwa na msemaji wake akituma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na serikali  ya Chad huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Halikadhalika Ban ameisifu Chad kwa ujasiri wake katika vita dhidi ya magaidi wa Boko Haram akisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Afrika ya Kati na Afrika Magharibi ili viwe thabiti zaidi.

Kwa mantiki hiyo amekaribisha maendele chanya ya kutekeleza kwa vitendo kikosi cha pamoja cha mataifa dhidi ya Boko Haram.

Hata hivyo Katibu Mkuu amesisitiza kuwa nchi zinapaswa kuzingatia wajibu na sheria za kimataifa za kibinadamu na za wakimbizi pindi zinapotekeleza mashambulizi dhidi ya kikundi hicho.