Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi dhidi ya Ntaganda kusikilizwa The Hague badala ya Bunia:ICC

Kesi dhidi ya Ntaganda kusikilizwa The Hague badala ya Bunia:ICC

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC imeamua kuwa kesi dhidi ya Bosco Ntaganda itasikilizwa makao makuu ya chombo hicho ambayo ni The Hague, Uholanzi.

Uamuzi huo wa leo umefanyika baada ya kutathmini pendekezo la tarehe 19 mwezi Machi mwaka huu kutoka jopo la majaji la kutaka usikilizaji wa awali wa kesi hiyo ufanyike huko Bunia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Jopo la majaji lilitaka usikilizaji uanzie huko Bunia ili kuwa karibu na wahanga wa kesi husika lakini ushauri kutoka pande za mashtaka, wahanga na kitengo cha usajili wa kesi ICC umelazimu kuamua vinginevyo.

Mathalani ICC imesema ni wazi kuwa kufanyika kwa kesi hiyo Bunia kungekuwa na mashiko na hata mtazamo lakini masuala kama vile gharama kubwa ya kuhamishia kesi huko Bunia na usalama wa mashuhuda kuwa mashakama vimeonekana kuwa na uzito zaidi.