Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi mwema wa UNICEF David Beckham ziarani Cambodia

Balozi mwema wa UNICEF David Beckham ziarani Cambodia

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF mwanamichezo David Beckham yuko ziarani nchini Cambodia ambapo atatathimini namna UNICEF inatoa usaidizi kwa watoto ambao wamekumbana na ukatili wa kimwili, kijinsia n ahata kihisia pamoja na ulinzi kwa watoto walioko katika mazingira hatarishi.

Taarifa ya UNICEF inasema kuwa huu ni mwendelezo wa harakati za mwanandinga huyo ambaye mapema mwka huu huu alizindua mpango uitwao namba 7 ambao ni mfuko wa David Beckman na UNICEF wa kulinda watoto walio hatarini .

Mwanasoka huyo ameahidi kutumia sauti yake kimataifa,pamoja na ushawishi kuchangisha fedha na kuhamasisha viongozi kote duniani kutengeneza mazingira ya mabadiliko chanya kwa watoto

Mfuko huo utasadia UNICEF katika kutekeleza mipango ya mabadiliko ya maisha kwa watoto duniani ikiwamo wale walioathiriwa na ukatili nchini Cambodia.

Akiwa ziarani nchini humo Beckham amesema anatarajia kukutana na watoto waliokabiliana na ukatili kusikiliza simulizi zao, na kuona kile kinachofanywa na UNICEF na washirika nakuongeza kuwa inasikitisha kuona kuwa kila dakika tano mtoto hufariki kutokana na ukatili na kutaka hilo kukomeshwa hima.