Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafugaji kuku Jamaica watambua faida za nishati mbadala

Wafugaji kuku Jamaica watambua faida za nishati mbadala

Gharama ya nishati inayoagizwa kutoka nje ni tatizo kubwa kwa wafanyabiashara nchini Jamaica. Asilimia 90 ya nishati inayotumiwa kwenye kisiwa hicho cha Bahari ya Karibe, huagizwa kutoka nje ya nchi.

Hii ina maana kuwa, biashara zote zinazotegemea nishati ya umeme, zikiwemo ufugaji kama wa kuku, hutumia pesa nyingi zaidi kwa mafuta na umeme, kuliko uwezo wao unavyokidhi. Lakini msukumo mpya wa matumizi ya nishati mbadala itokanayo na mionzi ya jua, umekuwa ukitolewa na Benki ya Dunia, kwa matarajio ya kukisaidia kisiwa hicho kukua zaidi.

Katika Makala hii, Joshua Mmali anatupeleka hadi kwa mfugaji mmoja wa kuku, karibu na mji wa St. Catherine, Jamaica.